Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania

Tanzania emblem

Karibu

Unakaribishwa kuja kuwekeza Nchini Tanzania, moja ya Nchi ambayo uchumi wake unakua kwa kasi katika Afrika. Tanzania imerahisisha sana mazingira ya biashara hasa katika maliasili na vivutio vingine vingi vinavyopatikana kwa ajili ya Uwekezaji.

Tanzania ni Nchi ambayo uchumi wake umeimarika na kukua kwa kasi ya asilimia saba (7%) kwa muda mfupi na imeweza kupanda kutoka katika Nchi zenye uchumi wa chini na kuwa katika Nchi yenye Uchumi wa kati duniani kwa mujibu wa taarifa rasmi ya benki ya dunia ambayo ilitolewa mnamo tarehe moja mwezi wa julai mwaka elfu mbili na ishirini (1 Julai, 2020). Mafanikio haya yamefikia miaka mitano kabla ya muda ambao ilitarajiwa kutokana na mpangokazi wa Taifa wa maendeleo ya mwaka 2025.

Hata hivyo ni dhahiri kwamba mafanikio haya yametokana na sekta mbalimbali kama vile Viwanda, miundombinu, huduma za kijamii,madini, ardhi pamoja na huduma bora za kijamii pia na usimamizi bora na wezeshi wa Serikali ya Tanzania.

Ili kuwa na mwendelezo na kuhakikisha mafanikio ya Uchumi wetu, Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anasisitiza mabadiliko ya uchumi wa viwanda ili kuvutia mazingira bora ya kisekta katika uwekezaji nchini.

 Sekta ya uzalishaji nchini imepewa kipaumbele Zaidi ilikuvutia wawekezaji nchini Tanzania hususani katika kuanzisha viwanda ambavyo vitazalisha bidhaa kwa kutumia malighafi zinazozalishwa ndani kama vile kusindika mazao ya kilimo. Mf. Miwa, korosho, pamba na korosho. Uzalishaji wa mafuta ghafi ya kula utokanao na mbegu za mazao kama vile Alizeti, Pamba, ufuta, karanga na mawese. Pia kuweza kuzalisha matunda na mbogamboga ambazo zitapelekwa katika mauzo ya nje ya nchi. Uvuvi wa samaki pamoja na usindikaji wake, mifugo, uchimbaji wa madini na pia uzalishaji wa vitu vya thamani vitokanavyo na madini hayo na mwisho kabisa ni uzalishaji wa vifaa tiba na maabara za kisasa.

Kutokana na maboresho bora na mageuzi ya kiuchumi. Tanzania imeweza kupata mafanikio ya uwekezaji katika Nyanja mbalimbali kutokana na taarifa ya RMB (Rand Merchant Bank) Kama inayoonyesha ni wapi kwa kuwekeza yaani (Where to Invest in Africa 2019) ambayo Tanzania imekua ya saba kati ya Nchi hamsini na nne za Afrika. Kingine cha muhimu zaidi ni kwamba Tanzania ndio Nchi pekee yenye Amani na utulivu katika umoja wa Nchi za Afrika Mashariki na pia ni ya hamsini na nne Duniani kulingana na taarifa ya dunia ya mwaka 2019 (Global Peace Index).

Tovuti hii inasaidia kutoa miongozo na taarifa muhimu ambazo zitamsaidia muwekezaji pamoja na wadau wengine katika kuwekeza. Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) ni sehemu pekee ambayo ilikasmiwa rasmi na Serikali katika kuratibu na kuratibu shughuli zote za uwekezaji Nchini ilipoamua kuunganisha taasisi zote za kisekta ili kutoa huduma mahali pamoja (One Stop Shop Centre) ili kurahisisha na kuharakisha uwekezaji
 

KARIBU SANA!

Ndg. Gilead Teri
Mkurugenzi Mkuu (TISEZA)

Feedbacks

Mrejesho, Malalamiko au Wazo