Muhtasari
Sekta ya Madini Tanzania ni muhimu sana kwa kuwa inachangia sehemu kubwa ya mapato ya nje ya nchi. Serikali ina mpango wa kuifanya sekta hii kuchangia 10% ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025. Licha ya makampuni makubwa machache, sekta hii ina makampuni kadhaa ya kati na kundi la makampuni madogo ya uchimbaji madini. Madini muhimu ni pamoja na makaa ya mawe, shaba, almasi, dhahabu, nikeli, fedha, uranium na vito vya Tanzanite, ambavyo havipatikani popote duniani isipokuwa Tanzania. Ingawa ugunduzi wa sasa wa hazina kubwa za gesi unaweza kubadilisha mlingano/mtazamo, Serikali ilipanga kupeleka nishati ya makaa ya mawe ili kukabiliana na uhaba wa nishati.
Mambo muhimu ya haraka
- Uchakataji wa madini ya thamani na vito.
- Kuanzisha kiwanda cha kusafisha magadi huko Engaruka.
- Uzalishaji wa mtapo wa chuma na chuma huko Liganga.
- Uchakataji wa nikeli huko Kabanga; na
- Kuchimba Uranium huko Mkuju.
- Uwekezaji katika viwanda vya kuyeyusha madini.
Fursa Zinazopatikana
- Mauzo ya madini nje ya nchi yaliingiza dola bilioni 1.37 ya jumla ya thamani ya mauzo ya nje ya Tanzania mwaka 2015 (yaani 24%) huku dhahabu ikiwakilisha zaidi ya 90% ya mauzo ya madini nje ya nchi.
- Tanzania imejaliwa kuwa na aina mbalimbali za madini ya viwandani na madini ya thamani pamoja na vito.
- Madini hayo ni pamoja na chuma, soda ash, makaa ya mawe, udongo wa mfinyanzi, uranium na dhahabu.
- Tanzania ina aina mbalimbali za vito, ikiwa ni pamoja na zumaridi, ganeti, rubi, yakuti, tumalini na tanzanite.
- Nyingi ya rasilimali hizi zinasafirishwa nje ya nchi zikiwa ghafi bila kuchakatwa; hivyo kuinyima nchi ajira.
